Soma masharti yetu ya matumizi kabla ya kutumia jukwaa la Tuka Bongo.
Tuka Bongo ni jukwaa la kidijitali la masimulizi na hadithi za Kiswahili. Kwa kutumia jukwaa hili, unakubali kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi, au umepata idhini ya mzazi/mlezi.
Unahitaji kuingia kwenye akaunti yako kupitia Google ili kufikia baadhi ya huduma kama kununua sarafu, kufungua hadithi, na kuhifadhi maktaba yako.
Unawajibika kulinda taarifa za kuingia kwenye akaunti yako na kuhakikisha usalama wake.
Sarafu (coins) ni mali ya kidijitali inayonunuliwa kupitia jukwaa letu. Kila hadithi ina gharama yake ya sarafu inayotolewa wazi kabla ya kununua.
Sarafu zinabaki kwenye akaunti yako hadi utakapozitumia. Hazina tarehe ya kumalizika.
Mara baada ya kufungua hadithi kwa kutumia sarafu, unapata ufikiaji wa sehemu zote za hadithi kwa muda wa siku 60 (miezi miwili). Baada ya hapo, ufikiaji unafungwa na unahitaji kufungua tena.
Hakuna marejesho ya sarafu zilizotumwa au hadithi zilizofunguliwa. Tafadhali hakikisha unataka kununua kabla ya kuthibitisha.
Hadithi zote zilizopakiwa kwenye Tuka Bongo ni mali ya wamiliki wao. Hatiruhusu kunakili, kusambaza, au kutumia maudhui yoyote bila ruhusa ya mwandishi au Tuka Bongo.
Unaruhusiwa kusoma hadithi ulizofungua kwa ajili ya matumizi yako binafsi tu. Usambazaji wowote wa maudhui ni marufuku na unaweza kusababisha kufungiwa kwa akaunti yako.
Kushare hadithi kupitia jukwaa letu (share button) ni ruhusu, lakini usambazaji wa maudhui kamili (copy-paste, screenshots, downloads) ni marufuku.
Unakubali kutumia jukwaa kwa njia ya heshima na kulingana na sheria. Hatiruhusu mwenendo wowote wa ukiukaji, uongo, au udhalilishaji.
Hatiruhusu kuunda akaunti nyingi kwa lengo la kudanganya mfumo wa sarafu au kupata faida isiyo halali.
Tunaweza kufuta au kufunga akaunti yoyote inayokiuka masharti haya bila taarifa mapema.
Tuka Bongo inaweza kubadilisha masharti haya wakati wowote. Mabadiliko muhimu yataarifiwa kupitia barua pepe au ujumbe kwenye jukwaa.
Endelea kutumia jukwaa baada ya mabadiliko kumaanisha umekubali masharti mapya.
Kwa maswali kuhusu masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano.
Soma pia: